Siku ya michezo watoto wote huonekana kuwa wenye furaha

Siku za Jumamosi watoto wote hukusanyika kituoni hapo na kuweza kucheza pamoja, kama wanavyoonekana kwenye picha wakifurahia michezo.
Japo kuwa watoto wa kituo hiki wanaonekana kupenda michezo, huenda wakawa wanapungukiwa vifaa vya michezo vitakavyosaidia kuweza kugundua vipaji vya watoto hawa,na kufahamu ninani mwenye kipaji gani.
Na kwa kuwa watoto waliopo ni kuanzia darasa la kwanza hadi Form One, basi pia huu ndio umri mzuri pia wa kutambua ni mtoto yupi anakipaji kipi.
Hivyo basi  mdau wetu kama utaguswa na jambo hili tunakukaribisha kwa chochote na tutafurahi sana kupokea kifaa chochote cha michezo kutoka kwako. Mawasiliano yetu angalia kwenye Contacts hapo juu. Asante
Siku ya michezo watoto wote huonekana kuwa wenye furaha Siku ya michezo watoto wote huonekana kuwa wenye furaha Reviewed by MAKIMBILIO CHILD CARE on September 26, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.